Nilipofika Golgotha nikaiona huko neema kubwa kama mto, neema ya ajabu.
Neema ya Golgotha ni kama bahari kubwa, ne'ma tele na ya milele, ne'ma ya kutosha!
Nilipofika moyo wangu ulilemewa sana,
Sikufaamu bado vema neema yake kubwa.
Neema ya Golgotha ni kama bahari kubwa, ne'ma tele na ya milele, ne'ma ya kutosha!
3. Nilipoona kwamba Yesu alichukua dhambi, neema ikadhihirika, na moyo ukapona.
Neema ya Golgotha ni kama bahari kubwa, ne'ma tele na ya milele, ne'ma ya kutosha!
4. Mbinguni nitakapofika, furaha itakuwa kuimba juu ya neema milele na milele.