Back to Top

Fresh Jumbe - Kizabizabina Lyrics

Fresh Jumbe - Kizabizabina Lyrics

Kizabizabina mwana wa hali kipi kikusikitishacho
Yakupatayo leo ndiyo matunda ya juhudi zako
Kama juhudi hizo ungezitumia kwenye kazi ungekuwa mtu wa maendeleo sana
Lakini leo kila upitapo watu wanakusema

Kaja kaja miguu ya ufagio eeh kaja kaja miguu ya ufagio eeh
Fanya uondoke utawaudhi wenzio eeh

Unanisikitisha ndugu yangu we kwa tabia uliyonayo ya ufagio
Kufagia lililo lako na lisilo la kwako
Umefanya watu wakupachike majina wengine wanakuita kizabizabina
Na wengine wanakuita mdaku wa kudakuwa

Umekuwa mtu wa kuhangaika huku na kule kutafuta mambo ili uyachukue
Madogo hata makubwa yote kwako wewe ni sawa
Ukishayapata unaongeza chunvi na pilipili na kuyapeleka kule sehemu ya pili
Watu wakigombana kwako wewe ni furaha

Sasa jamaa wamekushitukia wanakumulika kila unapozamia
Kila unapokwenda jamaa wamekupania
Hawana haja ya kukupiga wala kukuvamia bali ni kukucheka na kukuachilia
Na unapotokea wao wanakukimbia

DAR ES SALAAM hawakutaki
MOROGORO wamekuchoka
TANGA wamekususa umbea umekuzidi
UNGUJA NA PEMBA wahawakutaki
MAFIA wamekuchoka
NA MTWARA YOTE wamekususa umbea umekuzidi

Sasa umegunduwa kuwa ulipofikia ni pabaya yaya aah
Unaanza kujifaragua na kujikombakombakomba kwangu
Kujipitishapitisha na kujichekeshachekesha kwangu hakukusaidii
Kutaka urafiki na mimi ukidhani sijui mambo yako hello umekwama leo

MWANANYAMALA hawakutaki
KINONDONI wamekuchoka
OYSTERBAY wamekususa umbea umekuzidi
MAGOMENI hawakutaki
MSASANI YOTE wamekuchoka
MPAKA UBUNGO wamekususa umbea umekuzidi

Kwahiyo ushauri wa pekee nitakaokupatia mwana wa halali we
Ni kujaribu kurekebisha tabia yako na kuishi vyema na watu wa mitaani
Badilisha tabia yako badilisha mwenendo wako badilisha mfumo wa maisha yako
Na ukifanikiwa kubadilika nasi tutakupokea ayaya ayaya mmh

NA ILALA hawakutaki
KARIAKOO YOTE wamekuchoka
MPAKA CHAN'GOMBE wamekususa umbea umekuzidi
BUGURUNII hawakutaki
VINGUNGUTI wamekuchoka
MPAKA GONGO LA MBOTO wamekususa umbea umekuzidi

Hello hello kizabizabina wewe
Utakuwa mgeni wa nani sasa uko kwenye matatizo fikiria
Unaendekeza majungu fitina na unafiki tu
Hivyo upende usipende utake usitake nakwambia acha uzabizabina

MAKORORA hawakutaki
USAGARA YOTE wamekuchoka
NGAMIANI wamekususa umbea umekuzidi
MSAMBWENI hawakutaki
NA MAJENGO YOTE wamekuchoka
MAPINDUZI wamekususa umbea umekuzidi
BUYUNI KITOPENI hawakutaki
BAGAMOYO wamekuchoka
MPAKA PANGANI wamekususa umbea umekuzidi
MOSHI NA ARUSHA hawakutaki
DODOMA NA MWANZA wamekuchoka
HATA SHINYANGA wamekususa umbea umekuzidi

Daudi ni mtoto wa kanisani lakini ni mwana mpotevu hebu piga gitaa
Hello hello kizabizabina umekwama leo mama
Umekwama sababu ya tabia yako ooh

Mmmmmmmmmm! mh! wacha!
Hello, hello kizabizabina umekwama leo mama
Kumbe ni wewe Daudi
Mwana mpotevu piga gitaa
Bob Chipembe Saidi Chipembe mwambie Ali Juma Kizaizai anisalimie Malaika Maua

Angalia jamii inakutenga leo

Utamlilia nani huna rafiki

Walikuonya kuhusu tabia yako

Mmmmmmmmmmmmm!

Ukajiona wewe ni operator

Kuwaunganisha watu kwa mabaya yao

Ukajifanya wewe ni speaker

Kuyasema yasiyokuhusu

Kujifanya wewe ni mpelelezi

Kuchunguza yasiyokuhusu
[ Correct these Lyrics ]

[ Correct these Lyrics ]

We currently do not have these lyrics. If you would like to submit them, please use the form below.

Writer: Fresh Mkuu
Copyright: Lyrics © O/B/O DistroKid

Back to: Fresh Jumbe

Fresh Jumbe - Kizabizabina Video
(Show video at the top of the page)

Performed By: Fresh Jumbe
Length: 8:01
Written by: Fresh Mkuu
[Correct Info]
Tags:
No tags yet