Mapambano yameanza - Tuna pambana na Ukimwi
Nahatujui yatakwisha lini, mapambano - Ni vita mtindo mmoja hakuna kuchoka Ah
Mapambano hayo
Hatutashinda kama hatukushirikiana wote
Sikia Ah!
Vita kubwa tuliyonayo nikupambana na maradhi ya ukimwi
Na silaha zetu tulizonazo ni uaminifu na kuelewa kwa makini
Ni vipi utajikinga na ugonjwa huo maana haujapata dawa
Na vipi tutawaelimisha watoto wetu wasipatwe na balaa hilo
Vita hii ni kubwa tunapaswa kushirikiana kwa kushauriana
Tubadilishe tabia zetu katika jamii yetu kama tunataka kuishinda vita hii iiih aah yayayah!
Tusiwanyanyase waathirika - Hapana
Kwani wao hawakuomba ni bora tuwe nao
Kwa hali na mali tuwasaidie yoh
Tuzisaidie familia zao - Masikini
Kwani wao hawana nguvu tena za kuwatunza
Kwa taarifa kamili tulizozipata
Toka kwa wataalam waliosifika
Asilimia sabini duniani ya walioupata
Au kuathirika ni watu wa Africa
Ni wajibu wetu sasa kuingia kwenye vita
Si vya mabomu bunduki wala ndege za vita
Bali kuhakikisha tabia njema tunazifuata
Na kufuata ushauri nasaha tunaoupata
Mapambano yameanza - Eeeh
Nahatujui yatakwisha lini mapambano - Maa loo loo mapambano
Mapambano hayo - mmmh!
Hatutashinda kama hatukushirikiana wote
Kunusurika si ujanja na kuathirika si ujinga
Muhimu ni kuwapa upendo wale waathirika ili kuwapa faraja
Na kutoa mafunzo zaidi kwa wanusurika ili kuinusuru jamii
Na tujilinde wenyewe tukilinde kizazi kipya na pia tukilinde kizazi kijacho
Mliokwisha athirika muangalie vizuri
Msije mkawapaka wasiokuwa na habari
Kama mtu akikutaka muelezee dhahiri
Kwamba mimi nisingetaka kukuonjesha shubiri - ah
Tusiwanyanyase waathirika
Kwani wao hawakuomba ni bora tuwe nao
Kwa hali na mali tuwasaidie yoh
Tuzisaidie familia zao kwani wao hawana nguvu tena za kuwatunza
Mmmh aeh!
Mapambano yameanza nahatujui yatakwisha lini mapambano
Mapambano ya kupambana na Ukimwi yoh
Mapambano hayo hatutashinda kama hatukushirikiana wote