Penya moyo wangu nikujue zaidi
Ili moyoni mwangu kutiririke nyimbo za sifa
Penya moyo wangu nikujue zaidi
Ili moyoni mwangu kutiririke nyimbo za sifa
Yale niliyopitia yale ninayopitia,
Yale nitayopitia yanielekeze kukupa sifa
Penya moyo wangu nielimishe neno
Ili ndani yangu kutoke ibada ya sifa
Penya moyo wangu nikujue zaidi
Ili moyoni mwangu kutiririke nyimbo za sifa
Penya moyo wangu nikujue zaidi
Ili moyoni mwangu kutiririke nyimbo za sifa
Katika hali zote, unikumbushe Baba
Nisilalamike nikupe sifa na utukufu
Katika hali zote nisaidie Baba
Nikusujudu Wewe nikupe sifa na utukufu
Penya moyo wangu ewe mfinyanzi wangu
Ili ndani yangu nikuabudu nikupe sifa
Penya moyo wangu nikujue zaidi
Ili moyoni mwangu kutiririke nyimbo za sifa
Penya moyo wangu nikujue zaidi
Ili moyoni mwangu kutiririke nyimbo za sifa
Niundie moyo safi utokao sifa
Niinue jina lako nyakati zote Baba yangu
Natamani moyo safi unaonyenyekea
Mbele zako Baba moyo unaokuinua
Nikuabudu Baba nikupe sifa Yesu
Ninyenyekee kwako Muumba wangu pokea sifa
Penya moyo wangu nikujue zaidi
Ili moyoni mwangu kutiririke nyimbo za sifa
Penya moyo wangu nikujue zaidi
Ili moyoni mwangu kutiririke nyimbo za sifa
Penya moyo wangu nikujue zaidi
Ili moyoni mwangu kutiririke nyimbo za sifa
Penya moyo wangu nikujue zaidi
Ili moyoni mwangu kutiririke nyimbo za sifa
Penya Baba moyoni mwangu ninakungoja eeh (Penya)
Yesu wangu njoo upenye ndani eeh (Penya)
Jabali langu Wee kimbilio penya ndani aah (Penya)
Nimefungua moyo wangu upenye ndani eeh (Penya)
Mwokozi wangu nakutumai Baba yangu eeh (Penya)
Msaidizi wangu katika vita nisaidie (Penya)
Ili ndani yangu kutoke ibada ya sifa (Penya)
Nikuabudu nikuinue Mungu wangu Baba (Penya)
Nisujudu jinalo eeh Mungu wangu Yesu eeh (Penya)
Liinuliwe kula mahali duniani kote (Penya)
Aah Penya penya moyo wangu (Penya)
Aah Penya penya moyo wangu (Penya)
Baba Yangu