Wakati mwingine ni bahati tu
Upendo unapochipuka kwenye moyo
Uwepo wako unajazwa na neema isiyo na kifani
Utachukua muda mwingi
Ukijaribu kufafanua yote yanayokutendekea
Na yote unayohisi
Upendo upo tu
Upo katika mziki
Upo kwenye miti
Upo kwenye upepo tunapo barizi
Upendo upo wakati tunazaliwa hadi siku yetu ya Kufariki
Upendo upo ndani yangu
Kama vile mbegu kwenye tunda lake