Inawezekana umeona
Tumaini kwako halipo tena
Na inawezekana umeomba
Umeonda mbingu zimenyamaza kimya
Na umetafuta msaada
Hujaona pa kukimbilia
Ila yupo mwamba salama
Simba wa Yuda
Anasema njooni kwangu
Nyote msumbukao na mizigo
Anasema njooni kwangu
Nyote msumbukao na kulemewa na mizigo
Hufanya magumu kuwa rahisi
Hufanya mazito kuwa mepesi
Ni Yesu, Yesu
Hufanya magumu kuwa rahisi
Hufanya mazito kuwa mepesi
Ni Yesu, Yesu
Hufanya magumu kuwa rahisi
Hufanya mazito kuwa mepesi
Ni Yesu, Yesu
Hufanya magumu kuwa rahisi
Hufanya mazito kuwa mepesi
Ni Yesu, Yesu
Haijalishi muda gani umeomba
Umetafuta bila msaada
Yeye si kiziwi asisikie
Si kipofu, anaona
Anaelewa uwazavyo
Anasikia uombayo
Hachelewi wala hawahi
Anaelewa uwazavyo
Anasikia uombayo
Hachelewi wala hawahi
Huyu ni Mungu msikivu
Ni Mungu mwaminifu
Ni Mungu wa majira
(Huyu ni Mungu)
Mtoshelevu
Hufanya magumu kuwa rahisi
Hufanya mazito kuwa mepesi
Ni Yesu, Yesu
Hufanya magumu kuwa rahisi
Hufanya mazito kuwa mepesi
Ni Yesu, Yesu
Hufanya magumu kuwa rahisi
Hufanya mazito kuwa mepesi
Ni Yesu, Yesu
Hufanya magumu kuwa rahisi
Hufanya mazito kuwa mepesi
Ni Yesu, Yesu